[Verse 1: Diamond Platnumz]
Hhhhmm!
Ah! Leo Chereko chereko
Mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Ahsante mama ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua
Tena si kwa nazi
Si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama
Tu na dua
Waambie paparazi
Pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Ooooh! Oh!
[Chorus : DIamond Platnumz]
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana
Iyena Iyena (Aah ooh)
Iyena Iyena (Aah Iyeena)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
[Verse 2 : Diamond Platnumz]
Ooh! Ndoa baraka
Ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka
Kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia
Niushinde ujana
Ili kesho mahususi
Kusudi wasinong'one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi
Nakuvisha waone
Wakale sumu
Wavimbe wapasuke
[Bridge : Diamond Platnumz & Rayvanny]
Eeh!
Ati nashika nanga
Nteke nsichomoke ndani (Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani (Anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani (Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani (Anameremeta)
[Chorus : DIamond Platnumz]
Iyena Iyena (Aah iyoyo)
Iyena Iyena (Aah Eeeh)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Oh! Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena (Iyeeena)
Iyena Iyena (Aah Eeh)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
[Verse 3 : Rayvanny]
Imefika tamati
Tulisubiri kitambo
Leo samaki
Kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati
Yanavutia mapambo
Napata picha safi
Litanikoma bundle
Mwanamke usafi
Gaga kulisugua
Mume akirudi sharti
Viatu kumvua
Kitandani marashi
Massage kumchua
Kisha anza sayansi
Viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa
Si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa
Mumeo aone shanga
[Bridge : Rayvanny]
Eeeeh!
Makeup kinanda
Kaka suit kama mbunge (Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje (Anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na Fumbwe (Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (Anameremeta)
[Chorus : DIamond Platnumz]
Iyena Iyena (Aah iyeee)
Iyena Iyena (Aah iyoyo)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Eh! Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena (Iyeee)
Iyena Iyena (Hhhmm)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
[Outro : Diamond Platnumz & Rayvanny]
Saa nataka kusasambua (Sasambu)
Me nasasambua (Sasambu)
Aby Dad nasasambua mimi (Sasambu)
Sasambua!
Tuone
Mguu moja juu (Sasambu)
Usishushe chini (Sasambu)
Cheza jitazame (Sasambu)
Sasambua!
Tuone
Aisha kimobitel (Sasambu)
Nipe za baloteli (Sasambu)
Nyonga kibaiskeli (Sasambu)
Sasambua!
Tuone
Akaa kama unashika ukuta (Sasambu)
Ifanye unashusha (Sasambu)
Taratibu zungusha (Sasambu)
Sasambua
Tuone
Sasambu! Sasambu! Sasambu!
Sasambua!
Tuone
Kama unawasha bajaji (Sasambu)
Imwagie na maji (Sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (Sasambu)
Sasambua!
Tuone
Nyashinski "Hayawani" Kabla Swala ukamilishe Mama Tafadhali Mola mwambie Milele anichunge mi nisije zama Mashetani yasinivamie Chuki,wivu tunakutesa Linda kwako usiwaskie Kwa nini hatuwezi sote kupenda Oii wenzangu acha niwaambie Labda si sote wendawazimu! Labda laana yetu pesa Kesho ukipoteza kila kitu Dunia nzima itakucheka Wanaomba ntiliwe chai yangu sumu Wabaki hao ndio kusema Kesho wapigie demu wangu simu Asahau alivyonipenda! Oooh na mahayawani Hayayayaya Hayawani hawa wana si watu hawa Hayayayaya Binadamu kageuka mnyama! Hayawani hayawani hayawani Hayawani, hayawani hayayayaya Hayawani hayawani hayawani Hayawani, hayawani hayayayaya Tunaongezea nini bidii? Na roho ya mwanadamu haitosheki aki Sorry if I never made u happy I can't be there for everybody It's easy to see Wengi huishi kutafuta kasoro kwako Why man so money minded You wanna take from everyone Man eat man society Huoni haya kuvunja familia Hamna utu ni kujifikiria...
Comments
Post a Comment